7/7/16

LHRC Yaponda Bunge la Bajeti


KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema Bunge la 11, la kikao cha bajeti kilichomalizika Juni 30, mwaka huu, mjini Dodoma, lilishindwa kutoa uwakilishi kwa wananchi, kukosa umoja na ukiukwaji mkubwa wa kanuni za bunge.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Imelda-Lulu Urio.
Aidha, kimesema kituo hicho kimedai kiti cha Spika kilishindwa kusimamia kikamilifu kiti hicho na kusababisha vitendo vya matumizi mabaya ya muda wakati wa uchangiaji na wabunge kushindwa kuisimaia serikali.
Kimesema uongozi wa bunge akiwamo spika, naibu spika, wenyeviti ulitakiwa kusimamia kanuni, taratibu za bunge na kufanya maamuzi ya haki na kuweka maslahi ya taifa mbele.
Hayo yamo katika taarifa ya tathmini kuhusu bunge hilo la bajeti, iliyosomwa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Imelda-Lulu Urio.
Alisema tathmini hiyo ya awali kabla ya kutolewa kwa taarifa rasmi itakayokabidhiwa bungeni, imeonyesha kuwapo kwa changamoto nyingi katika bunge hilo, ikiwamo wananchi kunyimwa haki ya kujua hoja zinazowasilishwa bungeni kwa mujibu wa Katiba, ibara ya 18 (b).
“Bunge hili lilikuwa ni la wawakilishi wa wananchi lakini lenyewe limehariri taarifa za bunge kabla ya kuonyeshwa kwa wananchi tena katika muda ambao wengi wao hawakuweza kusikiliza wala kuangalia,” alisema Urio.
Alisema wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi walionyesha kutojitambua na kufahamu majukumu yao baada ya wabunge wa upinzani kutoka nje na kushindwa kuisimamia serikali hususan katika kashfa ya Lugumi na Escrow.
Urio alisema kutokana na wabunge wa upinzani kususia bunge, kulisababisha bajeti ya mwaka 2016/17 kupitishwa na wabunge 252 kati ya 384, hali ambayo imewanyima wananchi uwakilishi.
Alisema baadhi ya wabunge kutokuwa na imani na kumtaka Naibu Spika, Tulia Ackson ajiuzulu, kulionyesha kutokwenda sawa kwa shughuli za bunge ambazo spika anazisimamia, hivyo kunahitajika majadiliano ili kurejesha majukumu sahihi ya bunge.
Aidha, kituo hicho kimetaka kutengwa kwa bajeti rasmi kwa ajili ya kuendeleza mchakato wa Katiba mpya, ili kuboresha misingi ya mgawanyo wa madaraka na MWISHO
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts