Ligi ya China yazidi kumwaga fedha kwa mastaa wa soka | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

7/14/16

Ligi ya China yazidi kumwaga fedha kwa mastaa wa soka

Ligi kuu ya China (CSL) imeonekana kuanza kuzitesa ligi nyingine duniani kwa kumwaga fedha nyingi kwenye usajili.
13259043_231794520545897_881253747_n
Waswahili husema, “Penye udhia basi penyeza rupia” hicho ndicho kitu kimeonekana kwa matajiri wa China wakitaka kuivutia ligi yao iwe kubwa. Kutokana na hali isiyo ya kawaida kwa sasa wachezaji wengi maarufu wa soka wamekuwa wakikimbilia kucheza ligi ya China kutokana na fedha kibao wanazoahidiwa kupatiwa kwenye ligi hiyo.
Mastaa kibao akiwemo Ramires, Graziano Pelle, Hulk, De Mba, Gervinho, Jackson Martinez na wengine wengi wamezikimbia ligi kubwa za ushindani duniani na kwenda kwenye ligi hiyo ya China na kuanza kuingiza mkwanja mrefu.
13606666_974729799292195_3018764916184068271_n
Mpaka sasa Cristiano Ronaldo ndiye mwanamichezo mwenye utajiri mkubwa wa kiasi cha dola milioni 88 ambazo ni zaidi ya bilioni 190 za kitanzania.
Utajiri wa Ronaldo unatokana na mikataba kibao ya makampuni makubwa aliyonayo ikiwemo Nike, matangazo kupitia account zake za mitandao ya kijamii kama Twitter, Instagram na Facebook, manukato yake, na mikataba mingine mingi.

google+

linkedin