Linex: Yaliyotokea kati yangu na Adam Juma yalishapita | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

7/8/16

Linex: Yaliyotokea kati yangu na Adam Juma yalishapita

Muimbaji wa Moyo wa Subira, Linex amesema tofauti zilizojitokeza kati yake na Adam Juma ni mambo yaliyopita tayari.
13551655_507191039485683_1985723756_n
Linex alimtupia lawama AJ kuwa alilipua video ya wimbo wake ‘Mama Salima’ aliomshirikisha Diamond licha ya kumlipa bajeti ya kutosha.
“Binadamu hatuishi kwa mambo yaliyopita, tunaishi kwa wakati ambao upo na unaokuja,” Linex alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka.
“Wakati uliopita huwa ni kumbukumbu na history kwahiyo hatutakiwi kugombana tena mimi na Adam wala kutofautiana, wote tunakuwa hatujui mbele yetu kuna nini,” ameongeza.
Hivi karibuni muimbaji huyo aliachia wimbo wake, Hewala ambao anasema uongozi wake ndiyo wenye jibu sahihi nani ataiongoza huku Adam Juma akiwa miongoni mwa waongozaji watatu anaowafikiria.

google+

linkedin