7/22/16

Lowassa kumbukumbu pekee CCMWaziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa.Hatimaye Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete amezungumzia sakata lililotokea mwaka jana kwenye kikao cha Halmashauri Kuu baada ya jina la Edward Lowassa kuenguliwa kwenye mbio za urais ndani ya chama hicho, akisema chombo hicho ni kigumu na kinahitaji umakini katika kukiendesha.
Kikwete, ambaye leo anavua uenyekiti, alitumia sakata hilo kumtahadharisha mrithi wake, John Magufuli kuhusu uendeshaji wa chama hicho, hasa Halmashauri Kuu ambayo ni chombo cha pili kwa ukubwa baada ya Mkutano Mkuu.
Kikwete alitoa tahadhari hiyo jana alipokuwa akifungua kikao cha Halmashauri Kuu kilichohudhuriwa na wajumbe 365 kwenye ukumbi wa White House mjini hapa.
Kikwete aliwahakikishia kuwa baada ya CCM kuvuka mgogoro huo, sasa kimekuwa imara zaidi.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts