7/25/16

Makongoro Nyerere anusurika ajalini

 
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere amenusurika katika ajali baada ya gari lake kuwagonga ng’ombe saba kwenye eneo la Makatanini, Babati mkoani Manyara.
Mtoto huyo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa anatoka Dodoma kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM uliomchagua Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama hicho kwenda Arusha.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Francis Massawe amesema ajali hiyo ilitokea saa 1 usiku jana na kuwaua ng’ombe saba na kondoo mmoja.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo haikuwa na madhara ya binadamu, ni mifugo hiyo kuvushwa barabara sehemu isiyo na kivuko rasmi cha mifugo na katika tukio hilo. Mchungaji wa mifugo hiyo, William German alikimbia baada ya ajali hiyo
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm