7/20/16

Maonyesho ya 11 ya Vyuo vikuu vya Elimu ya Juu DSM

Serikali imesema imejipanga kuimarisha usimamizi wa utoaji wa elimu kwa vyuo vya elimu ya juu hapa nchini kutokana na kuwepo kwa vyuo vingi ambavyo vinakiuka matakwa ya serikali ikiwemo kuanzisha kozi ambazo haziruhusiwi kutolewa katika chuo husika hatua ambayo inawaathiri wanafunzi wanaosoma katika vyuo hivyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakati wa ufunguzi wa maonesho 11 ya vyuo vya elimu ya juu Waziri wa Elimu, Sayansi teknolojia na mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako amesema kwa sasa sheria ya vyuo vikuu haitoi fursa ya kuweza kuchukua hatua kwa vyuo vya kitapeli ambavyo vimekuwa vikitoa mafunzo katika ngazi ambazo hazistahili.

Aidha amezungumzia utaoji wa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi hewa ambapo mpaka sasa vyuo vitano vimefanyiwa uchunguzi.

Akizungumzia kazi zinazofanywa na chuo cha kilimo sokoine SUA mtaalamu wa sayansi ya udongo Elia Kmwela amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kujifunza kazi za vyuo hivyo ikiwemo tafiti mbalimbali zinazofanywa akitolea mfano matumizi ya mbolea kwa wakulima.

Maonyesho hayo yanayofanyika kila mwaka yamejumuisha vyuo kutoka mikoa yote tanzania bara na visiwani kwa lengo la kutoa fursa kwa wanafunzi kupata taarifa za vyuo vyote sehemu moja.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm