7/22/16

Mbwa Aokoa Binadamu Asiuawe na Chui Katika Hifadhi ya Serengeti

MTU mmoja, Makang’ha Mandazi (32), amenusurika kuuawa na chui aliyetoka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuvamia makazi ya watu katika kijiji cha Kihumbu, kata ya Hunyari, wilaya ya Bunda, mkoani Mara.
Mandazi mkazi wa kijiji hicho, alinusurika kifo baada ya mnyama huyo kumvamia nyumbani kwake juzi saa 4:00 asubuhi na kuanza kushambuliwa huku akiwa ameangushwa chini, lakini akaokolewa na mbwa wake aliyemng’ata mkia mnyama huyo hatari.
Akizungumzia tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi kijijini hapo, Diwani wa Kata ya Hunyari, Magina Josephat, alisema lilitokea katika kijiji cha Kihumbu.
“Alinusurika kifo baada ya kuokolewa na mbwa wake aliyemng’ata mkia mnyama huyo, hali ambayo ilipelekea kumwachia na kuanza kushambuliana wanyama wenyewe na kutoa nafasi kwa majeruhi huyo kukimbia kuokoa maisha yake,” alisema.  <<SOMA ZAIDI HAPA>>
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm