7/11/16

Mfalme wa Soka Pele Kuoa Mara ya Tatu

Mfalme wa soka duniani, Pele ametangaza kufunga ndoa kwa mara ya tatu akiwa na umri wa miaka 75.
Pele na mpenzi wake, Marcia .
Pele aliyetwaa kombe la dunia mara tatu akiwa na timu ya taifa ya Brazil, atafunga ndoa na mpenzi wake wa miaka sita, Marcia Cibele Aoki siku ya Jumanne, katika sherehe ndogo, kwa mujibu wa gazeti la O Estado de Sao Paulo.
Marcia Cibele Aoki mwenye miaka 42 ni mfanyabiashara na amekuwa akionekana pembeni ya Pele katika matukio tofauti tangu mwaka 2012, na hata pale gwiji huyo wa soka alipolazwa hospitalini mara kadhaa.
Ndoa mbili za awali za Pele kila moja ilidumu kwa zaidi ya miaka 10, ambapo kwenye ndoa ya kwanza alizaaa watoto watatu na ndoa ya pili watoto wawili.
Edson Arantes do Nascimento, Pele, wakati wa enzi zake alifunga jumla ya mabao 1,281 katika mechi 1,363, ambapo aliichezea timu ya taifa ya Brazil mara 91 kati ya mwaka 1957 hadi 1971 .
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts