7/1/16

Mgambo watakiwa kuzingatia sheria kwa wafanyabiashara

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imeziagiza halmashauri nchini kuhakikisha mgambo wanaotumika kuwafukuza wafanyabiashara wadogo wanazingatia sheria na kanuni.


Agizo hilo lilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo akisema Serikali katika maeneo husika hulazimika kuwatumia mgambo kuwaondoa wafanyabiashara na kuwaelekeza kwenda katika maeneo yaliyopangwa rasmi kwa shughuli zao.


Naibu Waziri alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mariamu Kisangi aliyetaka kujua Serikali inawasaidiaje wajasiriamali wadogo ambao hujipatia riziki zao kupitia biashara ndogo ndogo.


Naibu Waziri alisema Serikali inathamini mchango wa wafanyabiashara wadogo katika kukuza ajira na kipato.


Alisema wafanyabiashara wadogo wanatakiwa kuendesha biashara zao katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao na kwamba bado Serikali inaendelea kurasimisha biashara katika mfumo usiokuwa rasmi ili kuzitambua, kuzisajili na kuongeza mchango katika ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja.


Aliwashauri wafanyabiashara wadogo kuunganisha biashara zao na kuunda kampuni ndogo ili waweze kukopesheka katika taasisi za fedha na kuongeza tija katika biashara.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts