7/25/16

Mkuu wa wilaya aagiza kushughulikiwa kwa watumishi wenye lugha chafu hospitali ya Somanda.

 bariadi
Kufuatia malalamiko ya wananchi ya muda mrefu kuhusiana na  kukithiri kwa lugha chafu kwa wagonjwa zinazotolewa  na baadhi ya watumishi wa idara ya afya  katika hospitali ya Somanda  iliyoko ,halmashauri ya mji wa Bariadi, Mganga Mkuu  ameagizwa kuwaajibisha waliotajwa kuwa vinara wa vitendo hivyo.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga alipokutana na watumishi wa afya hospitalini hapo katika kikao cha pamoja ili kuwakumbusha wajibu na majukumu yao wanayopaswa kuyatekeleza wakiwa katika maeneo yao ya kazi ambapo  amesema ni lazima wawajibishwa wenye tabia hizo kwani kauli chafu dhidi ya wagonjwa zinawasababishia maumivu zaidi wagonjwa.
Ameongeza kuwa kazi ya Udaktari na watumishi wa afya kwa pamoja ni wito hivyo amewataka  kuacha mara moja tabia hiyo, na kuwataka kila mtu kufanya kazi kwa kuzingatia kanunu za utumishi wa umma ili kulinda kazi na nafasi zao.
Katika hatua nyingine ametoa wiki moja kuhakikisha hospitali hiyo iliyokithiri kwa uchafu, mazingira yake yawe katika hali ya usafi, ili kuepuka magonjwa ya milipuko.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa  halmashauri ya mji wa Bariadi Dkt Akilimali Mpozemenya  amesema kuwa maagizo aliyopewa atayafanyia kazi ,na tayari hatua zinaendelea kuchukuliwa.
Naye  katibu wa hospitali ya Somanda  Nusu Salum amekiri kuwepo kwa uchafu  ndani na nje ya hospitali hiyo na  kuhaidi kulifanyia kazi kwa kushirikiana na kampuni ya kufanya usafi iliyopo hospitalini hapo
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts