7/26/16

Mkwasa ameita wachezaji 24 Taifa Stars, bila uwepo wa Samatta na Ulimwengu

https://encrypted-tbn2.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcQodHzgMgbSi-9rIYliUHJxGa3gtSdwskWeKtOBvuJ20O74gV-Z
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa leo July 26 2016 ametangaza kikosi cha wachezaji watakaoanza maandalizi ya kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba wa michuano ya AFCON dhidi ya Nigeria, Mkwasa ameita kikosi hicho baada ya ombi lao la mchezo wao dhidi ya Nigeria kufutwa kukataliwa.
Wachezaji hao walioitwa na Mkwasa wanatakiwa kuripoti kambini July 31 2016 na kuanza kambi ya siku tano itakayomalizika August 5 2016, hata hivyo kuelekea mchezo huo wa Nigeria utakaochezwa mwanzoni mwa mwezi September utawakosa wachezaji wanaocheza soka nje ya nchi kama Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Magolikipa
Deogratus Munish, Beno Kakolanya (Yanga), Aishi Manula (Azam FC) Mabeki
Oscar Joshua,  Kelvin Yondani, Juma Abdul (Yanga), Erasto Nyoni, Agrey Morris (Azam FC) Mohamed Hussein (Simba ).
Viungo
Farid Musa, Himid Mao (Azam FC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude (Simba), Ibrahim Rajab ‘Jeba’ (Mtibwa Sugar ), Hassan Kabunda (Mwadui FC), Simon Msuva, Juma Mahadh (Yanga ).
Washambuliaji
Joseph Mahundi (Mbeya City), Ibrahim Ajib, Jamal Mnyate (Simba), John Bocco (Azam FC) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts