Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

7/1/16

Mlowola: Ndoto Yangu Ilikuwa kuwa Padri

Kupitia historia watu wamekuwa wakiamini kuwa ndoto nyingi zina maana fulani. Lakini kisaikolojia ndoto imekuwa ikielezwa kuwa ni uwajibikaji wa asili wa kiakili wakati wa usingizi.


Si lazima ukiwa usingizini ndio upate ndoto. Hata ukiwa katika shughuli zako za kila siku unaweza kuwa na ndoto ya kuwa mtu fulani katika jamii inayokuzunguka.


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola alikuwa na ndoto ya kuwa Padri wa Kanisa Katoliki kabla ya kukatishwa ndoto zake na kuamua kujiunga na Jeshi la Polisi.


Mlowola ambaye ni mkurugenzi wa sita kuiongoza taasisi hiyo anayeamini kuwa rushwa ni tatizo kubwa zaidi nchini kuliko ugaidi, anasema wakati huo akisoma seminari alielezwa kuwa upadri haumfai kwa sababu ya mambo mawili tu; eti alikuwa akipenda sana muziki na mpira wa miguu.


Akizungumza Alhamisi iliyopita katika mahojiano maalum na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam, huku akiwa pamoja na wasaidizi wake, Mlowola ambaye kipaji chake katika soka kilimfanya acheze ligi daraja la pili ngazi ya mkoa, anasema kama angefanikiwa kuwa Padri hivi sasa huenda angekuwa Askofu wa jimbo fulani nchini.


Mlowola ambaye aliteuliwa Desemba 4, 2015 kukaimu nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Dk Edward Hoseah kabla ya kuteuliwa rasmi, alionekana kulifurahia swali lililomtaka aeleze kazi ambayo angeifanya kama asingejiunga na Jeshi la Polisi.


Mkurugenzi huyo ambaye wasaidizi wake walikuwa wakirekodi mazungumzo yake na waandishi wa gazeti hili anajibu, “Ningekuwa padri, nilisoma seminari na mpaka sasa ningekuwa askofu. Niliambiwa kuwa nimekosa mwito ila sikukubaliana nao.”


Kwa nini aliambiwa amekosa wito?


Mlowola anasema hiyo ilitokana na jinsi uongozi wa Kanisa unavyomfuatilia mtu anayetaka kuwa padri, wanaangalia mambo mengi ikiwa ni pamoja na historia ya familia.


“Wenyewe wanakuona. Mimi nilikuwa napenda kucheza mpira na muziki. Na dhani suala kubwa lilikuwa muziki.


“Kwa sababu babu yangu nasikia alikuwa kiongozi wa bendi ya kwanza kule uswahilini kwetu nikahusishwa moja kwa moja na mambo ya muziki,” anasema Mlowola.


Anasema baada ya kukatishwa ndoto zake katika upadri, aliutamani muziki na alitaka kuwa mwanamuziki, tena mpiga gitaa la besi.


Katika soka, Mlowola anasema alicheza ligi daraja la pili, timu ya Chuo cha Polisi Moshi (CCP) na kushiriki mara kadhaa michuano ya shule za sekondari nchini (Umiseta).


Si Mlowola tu aliyeutamani upadri. Juni 2, mwaka huu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simona Sirro katika mahojiano maalum na gazeti hili alisema ndoto yake ilikuwa kuwa padri lakini ilikatishwa na wazazi wake waliomtaka aoe.


Rushwa na ugaidi


Mlowola ambaye amewahi kuwa Kamishna wa Polisi na Mkurugenzi wa Intelijensia ya Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi anasema: “Nikiri kabla ya kufikia Takukuru nilikuwa polisi, moja ya mambo niliyokuwa nashughulikia ni mikakati ya kupambana na ugaidi Tanzania.


“Nilikuwa nadhani wakati ule tatizo linaloathiri usalama wa nchi yetu na dunia ilikuwa ugaidi, lakini baada ya kuja Takukuru nimegundua kuwa tatizo kubwa kwa Serikali ni rushwa.”


Anasema uuzaji wa dawa za kulevya ukikithiri lazima kuna rushwa nyuma yake, hivyo hivyo katika ujangili na sekta ya ujenzi.


“Ujangili unafanyika kutokana na kushamiri kwa rushwa, katika sekta ya ujenzi ukiona majengo yanaanguka na barabara na madaraja kujengwa kwa kiwango cha chini ujue kuwa tatizo ni rushwa,” anasema.


Anasema licha ya kuwa tatizo la rushwa ni kubwa nchini, Takukuru inafanya jitihada za dhati za kupambana nalo, jitihada alizodai kuwa ni za kiwango cha juu kuliko ilivyokuwa zamani.


“Siri kubwa ya mapambano dhidi ya rushwa duniani yanategemea sana utashi wa kisiasa. Unaweza kuwa na sheria, taasisi nzuri, lakini ukikosa utashi wa kisiasa mapambano yote ya rushwa hayatakuwa na nguvu,” anasema.


Ukubwa wa rushwa Tanzania


Anasema tatizo la rushwa nchini ni kubwa na ndiyo sababu wagombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita sambamba na vyama vyao, ajenda yao kubwa ilikuwa ni kupambana na rushwa na ufisadi.


“Hii inamaanisha tatizo ni kubwa nchini ndiyo maana ilikuwa ajenda kuu ya kisiasa. Rais Magufuli aliahidi katika kampeni zake kuwa atapambana na ufisadi na kuahidi kuunda mahakama ya mafisadi. Hata Ukawa, ajenda yao ilikuwa ni ufisadi. Kila chama makini kilizungumzia ufisadi na maana yake tatizo la rushwa lilikuwa kubwa,” anasema.


“Taasisi mbalimbali zilifanya utafiti na kuonyesha hali hii ya rushwa nchini. Wanahabari nao mlizungumza na wananchi wa kawaida, mliona jinsi wanavyolalamikia rushwa katika huduma mfano za hospitali.”


Anasema tatizo la rushwa si Tanzania pekee bali ni la dunia nzima huku akitolea mfano jinsi rushwa ilivyozua mjadala katika mkutano wa wakuu wa nchi wa kujadili mapambano dhidi ya rushwa (Anti-Corruption Summit 2016) uliofanyika London, Uingereza.


“Katika mkutano ule (Anti Corruption Summit 2016) ambao Rais John Magufuli alialikwa, lakini akawakilishwa na Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa). Yeye (Rais Magufuli) pamoja na rais wa Nigeria walitambuliwa katika mapambano yao dhidi ya rushwa,” anasema.


Anasema katika mkutano huo rushwa ilionekana ni tatizo duniani na imeathiri hata masuala ya usalama.


Anasema kama uchumi wa Tanzania ukitoa tija ya kuweza kugharamia huduma za jamii kwa ufanisi zaidi, rushwa itapungua hasa rushwa ndogo kwa maelezo kuwa katika hospitali, shule na maeneo mengine ya kutoa huduma kila kitu cha msingi kitakuwapo.


“Kukiwa na huduma hafifu kunakuwa na kinyang’anyiro. Watu wenye nguvu watataka kupata kipaumbele, lakini wakati huohuo watumishi wa Serikali vipato vyao vidogo, hivyo watu wenye uwezo wanawarubuni watumishi ili wawape upendeleo,” anasema.


Ulafi wa viongozi


Kuhusu rushwa kubwa, Mlowola anatolea mfano mtu mwenye wadhifa wa uwaziri au ukurugenzi ambaye analazimisha kupata zaidi licha ya kuwa kipato chake ni kizuri.


“Kwa hali hii kampuni zinazotaka rasilimali zitakuhonga na wewe kwa sababu ya nafasi yako ukafanya mambo bila kujali maslahi ya nchi yako.


“Makampuni makubwa yanahonga viongozi wa Afrika ili wapate ulaji na sisi tunatumika hivyo na hilo ndio tatizo kubwa.”


Akizungumzia madai kuwa kesi za rushwa zinasuasua kutokana na kukosekana kwa ushahidi, Mlowola anasema jambo hilo si kweli kwa maelezo kuwa Takukuru inashinda kesi nyingi.


Hata hivyo anakiri kuwa kuna udhaifu katika upelelezi na pia katika upatikanaji wa mashahidi na tatu ni rushwa ni rushwa yenyewe kuingia hadi ndani ya vyombo vya kutolea haki.


Anasema kuna kesi za rushwa ambazo ushahidi wake una mlolongo mrefu na kuhusisha nchi zaidi ya moja jambo ambalo wakati mwingine huchukua muda mrefu na hatimaye kesi husika kutupwa.


“Unaomba ushahidi uko Australia na mlolongo wake ni mrefu lazima ipite kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Wizara ya Mambo ya Nje ya huko kisha waende kwa mwanasheria mkuu wa huko au DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka), watathimini, hivyo inachukua muda mrefu na kuna nchi ambazo ushahidi huo upo zina tabia ya kulinda makampuni yao,” anasema.


Anasema changamoto inayoikumba taasisi hiyo kwa sasa ni kupokea taarifa kwa kiwango kikubwa kutokana na msisitizo wa Rais katika kupambana na rushwa na ufisadi.


“Taarifa ni nyingi mno kiasi cha kushindwa kuzikabili na kutoa majibu ya haraka. Ila tunajipanga kukabiliana na hiyo hali hii. Ila changamoto nyingine zinatatulika,” anasema Mlowola.