7/2/16

Moto Wateketeza Vibanda

Moto umeteketeza vibanda zaidi ya 500 vya biashara visiwani Kabiga na Migongo wilayani Serengeti Mkoa wa Mwanza.

Moto huo umetokea katika matukio mawili tofauti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema leo kuwa katika Kisiwa cha Kabiga Kata ya Maisome zaidi ya vibanda 300 viliteketea Alhamisi wakati wafanyabiashara walipokuwa wakigawana mafuta ya petroli yanayodaiwa kuibwa.

Amesema mmoja wa wafanyabiashara hao aliagusha kipande cha sigara kilichowashwa ndipo moto ulipolipuka.

Amesema katika Kisiwa cha Migongo Kata ya Maisome, zaidi ya vibanda 200 viliteketea jana usiku chanzo kikiwa ni mshumaa.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts