Mr Blue adai wasanii wakongwe hawapewi heshima inayostahili | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

7/12/16

Mr Blue adai wasanii wakongwe hawapewi heshima inayostahili

Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue amedai kuwa mtindo wa kuwapa kipaumbele wasanii wachanga kuliko wakongwe kinawafanya wasanii hao wachukuliwe poa.
f1cbmr-Blue-ft-alikiba-mboga-saba
Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Television Jumatatu hii, Mr Blue amesema kitendo hicho kinawavunja moyo wasanii wengi wakubwa hali ambayo inawafanya wasanii hao kukata tamaa.
“Sio tu wasanii wakubwa hawafanyi vizuri, lakini wanapewa heshima inayostahili kwenye game?,” aliuliza Mr Blue. “Unakuta msanii ndogo ana nyimbo mbili lakini analipwa pesa nyingi kuliko msanii mkongwe, vitu kama hivi vinavunja moyo,”
Rapper huyo amewataka wadau mbalimbali wa muziki nchini kuwapa heshima wasanii wakongwe kwani kufanyahivyo ni kuijenga tasnia ya muziki.

google+

linkedin