7/22/16

Msanii Ismail Makombe (Kundambanda), Afariki Dunia


1
Msanii maarufu wa Vichekesho (Komedi)  kutoka  kundi la Vituko Show Ndugu. Ismail Issa Makombe a.k.a KUNDAMBANDA, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Kundambanda alikuwa mgombea ubunge wa CUF na UKAWA kwenye jimbo la Masasi – Mtwara katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Disemba 2015 baada ya ule wa Oktoba kutofanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa awali wa UKAWA, Mhe. Emmanuel Makaidi (NLD).
Katika uchaguzi huo wa Disemba 2015 Kundambanda alipata kura 14,069 dhidi ya kura 16,597 za (mshindi) Rashid Chua Chua kutoka CCM. Taratibu za mazishi zinafanyikia nyumbani kwao Masasi
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm