7/31/16

Muhagama: Tumeunda kikosi kazi kwenda kuandaa mazingira Dodoma


Waziri Ofisi ya Rais, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Jenista Muhagama amesema wizara yake imeandaa kikosi kazi kitakachotangulia kwenda Dodoma wiki ijayo kwa ajili ya kuandaa mazingira kabla ya wizara nyingine.
Muhagama amesema hayo usiku huu alipokuwa akizungumza katika kipindi maalumu kupitia Televisheni ya Taifa (TBC1) kilichoandaliwa na wizara hiyo.
Amesema bajeti zote za ujenzi wa majengo ama ofisi jijini Dar es Salaam zilizotengwa na wizara mbalimbali sasa zitajenga majengo hayo mkoani Dodoma.

mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts