7/30/16

Naibu Waziri wa Habari afungua mashindano ya brazuka kibenki


Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikagua timu wa wachezaji wa Diamond Trust Bank (DTB) wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mratibu wa mashindano hayo kutoka Barclays Bi. Nasikia Berya
Mchezaji kutoka timu ya Barclays akijaribu kuzuia mpira kutoka kwa mchezaji wa timu ya DTB wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wanamichezo kutoka mabenki mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi naodha wa timu ya DTB ngao ya hisani kwa kuwafunga mabao matatu kwa moja timu ya Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Michezo Bw. Rashid Mijuza.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati mwenye koti la bluu) katika picha ya pamoja na wachezaji kutoka Barclays wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki maarufu kama brazuka leo Jijini Dar es Salaam.
Waamuzi wa michezo ya Brazuka kibenki katika picha ya pamoja wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya kibenki leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu
Na: Lorietha Laurence
Serikali kupitia sera ya Maendeleo ya Michezo inasisitiza wananchi na jamii kwa ujumla kushiriki katika michezo ili kujenga afya, kuunganisha watu toka makundi mbalimbali bila ubaguzi wa kidini, kisiasa, wala kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati wa ufunguzi  wa mashindano ya Kombe la Kibenki maarufu kama Brazuka katika viwanja vya Gymkhana leo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Wambura ameeleza kuwa ni muhimu  kwa wafanyakazi  kujumuika kwa pamoja katika michezo ili kuboresha afya  na kuimarisha uhusiano baina yao.
“Michezo ni kitu kizuri kwani husaidia katika kuimarisha na kulinda afya zetu hivyo ni vyema kila mmoja wetu kushiriki katika michezo ili kuwa nguvu ya kutekeleza majukumu yetu ya kila siku” alisema Mhe. Wambura.
Vilevile alitoa shukrani  kwa wakuu wote wa mabenki kwa ushirikiano wao  wa kuwaleta pamoja wafanyakazi wa benki ili kufahamiana na kuimarisha ushirikiano baina yao.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Bw. Aron Luhanga amesema kuwa dhumuni la mashindano hayo ni kuendeleza mahusiano baina ya benki kwa kufahamiana na kuimarisha afya na fikra zao.
“mashindano haya ni kwa ajili ya kufahamiana na kuimarisha urafiki kwa wafanyakazi wa sekta ya benki kwa kufanya sekta ya kibenki kuwa sehemu bora ya shughuli za kiuchumi nchini” alisema Bw. Luhanga.
Mashindano hayo ya Brazuka kibenki  yanaratibiwa na  benki ya  Barclays na ni mara ya pili kufanyika nchini ambapo mwaka jana benki ya Diamond Trust (DTB) iliibuka mshindi hivyo kushiriki katika  ufunguzi wa michuano hiyo mwaka huu.
Benki zinazoshiriki mashindano hayo ni  18 ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania, NMB, Stanbic, KCB, Exim, Citi Benki, Commrcial Bank of Africa (BOA),CRDB, Letshego, Eco Bwnki, Akiba, Diamond Trust Benki, Bank of India, Banc ABC,Azania na Twiga Bancorp.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts