Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akutana na uongozi wa Radio Maarifa iliyopo Jijini Tanga. | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

7/20/16

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akutana na uongozi wa Radio Maarifa iliyopo Jijini Tanga.Mkurugenzi na mmiliki wa wa Redio Maarifa Bw. Mohamed Somji akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mazungumzo kuhusu kupata masafa ya kurusha matangazo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kushoto ni mtangazaji na mchambuzi wa mada katika Redio hiyo Sheikh Jalala leo Julai 20, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akizungumza  na uongozi wa Redio Maarifa kuhusu kupata masafa ya kurusha matangazo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo Julai 2016, katikati ni Mkurugenzi na mmiliki wa wa Redio Maarifa Bw. Mohamed Somji na kushoto ni mtangazaji na mchambuzi wa mada katika Redio hiyo Sheikh Jalala.

Mkurugenzi na mmilikiwa wa Redio Maarifa Bw. Mohamed Somji (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura Ofisini kwa Naibu Waziri kuhusu kupata masafa ya kurusha matangazo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam leo Julai 2016 kushoto ni mtangazaji na mchambuzi wa mada katika Redio hiyo Sheikh Jalala. .

Mkurugenzi na mmilikiwa wa Redio Maarifa Bw. Mohamed Somji akimuonesha Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura baadhi ya nyaraka za kibali cha awali cha kurusha matangazo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisini kwa Naibu Waziri leo Jijini Dar es Salaam Julai 20, 2016.

Afisa Habari Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Bw. Jonas Kamaleki (kushoto) akieleza umuhimu wa kufuata Sheria na maadili ya habari katika kufikisha ujumbe kwa jamii wakati uongozi wa Redio Maarifa ulipokutana na  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura kujadili kuhusu kupata masafa ya kurusha matangazo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo Julai 20,2016 Jijini Dar es Salaam.

 Mtangazaji na mchambuzi wa mada katika Redio Maarifa  Sheikh Jalala akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura wakati uongozi wa Redio Maarifa ulipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam Julai 20, 2016.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Redio Maarifa iliyopo Jijini Tanga walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo Julai 20,2016.
Picha  na Shamimu Nyaki

google+

linkedin