7/2/16

Nay Wa Mitego: nakerwa na wasanii wanaotafuta kiki kupitia malumbano.

Rapa Nay wa Mitego amesema kuwa anakerwa na tabia ya baadhi ya wasanii ya kuanzisha malumbano ili wapate nafasi ya kuandikwa katika vyombo vya habari kwa lengo la kupata umaarufu.
Alisema msanii aliyekamilika huandaa kazi zenye ubora na si kutegemea malumbano badala ya kujijengea,baadhi yao majina ‘huchafuka’ na kupotea kwenye gemu la muziki.
“Ninasema hivyo kwa sababu wapo wasanii wengi tu wamekuwa wakitafuta ‘kiki’ kupitia kwangu kwa kuanzisha malumbano,kwa sasa nimeshawagungua na sitaki kuwajibu,”alisema Nay Wa Mitego.
“kazi zangu ndizo zime ni weka juu hadi sasa,hivyo na wao pia wafanye juhudi kwa kutayarisha kazi zinazokubalika,watapa umaarufu ndani na nje ya nchini,njia ya malumbano haitawasaidia na si bora,msanii huyo aliongeza.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm