7/3/16

Ngoma: Tutafia Uwanjani Dhidi ya Medeama
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Donald Ngoma, amesema kuwa mchezo wao unaofuata wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana ni wa kufa na kupona.Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ngoma, alisema kuwa hawana chaguo lingine zaidi ya ushindi kwenye mchezo huo muhimu.

"Watu waanze kutuhukumu au kutucheka baada ya mchezo wetu na Medeama, ni lazima ushindi kwa sababu bila kufanya hivyo tukuwa tumejiangamiza," alisema Ngoma.

Alisema kuwa mashabiki wasiwe na shaka kwa kuwa wamejiandaa vyema kushinda mchezo huo.

"Watuamini tu,tumepoteza michezo miwili na kwa sasa hatufikilii hilo kutokea tena, tutacheza na Medeama huku tukifahamu kabisa ushindi ni muhimu kwetu," alisema Ngoma.

Nyota huyo raia wa Zimbabwe, ameshindwa kuzifumania nyavu katika michezo miwili hatua ya makundi waliyocheza mpaka sasa.

yanga imepoteza michezo yake miwili kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts