7/1/16

Omog awasili rasmi Simba

 Kocha mpya wa Simba, Joseph Omog akiwasili
Kocha mpya wa Simba, Joseph Omog amewasili alfajiri hii tayari kwa kuingia mkataba wa kuifundisha timu hiyo.
Baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Omog alipokewa na Katibu mpya wa Simba, Patrick Kahemele na kupelekwa moja kwa moja katika hoteli atakayofikia.
Kocha huyo ambaye awali aliifundisha Azam FC na kuipa ubingwa wa kihistoria, hakuzungumza chochote kutokana na kulalamika uchovu wa safari ingawa alionyesha kuwa na furaha huku akitamka kuwa amefurahia kurudi nchini kujiunga na marafiki zake wengine.
Omog, raia wa Cameron amewasili nchini majira ya saa 8:35 usiku akitokea kwao, leo anatarajiwa kutambulishwa rasmi na uongozi wa Simba zoezi ambalo litatanguliwa na tukio la kusaini
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm