Polisi Dar kuhusu kifungo anachoweza kupata mwenye kosa la mapenzi ya jinsia moja | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

7/9/16

Polisi Dar kuhusu kifungo anachoweza kupata mwenye kosa la mapenzi ya jinsia moja


Baada ya mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja kumekuwa na taarifa za mitandaoni kwamba tayari jeshi la polisi kanda maalum Dar es salaam limeshaanza kuwakamata baadhi ya Watuhumiwa.
AyoTV imempata kamanda wa Polisi kanda maalum Dar es salaam Simon Sirro aliesema >>>’Hili kosa lipo muda mrefu, ukienda kwenye sheria za adhabu kwa nchi yetu kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai na tumekuwa tukiwakamata watu
Kilichokuwa kinakosekana ni suala tu la taarifa lakini ukipatikana hukumu yake ni kubwa inategemea na hakimu, kama sikosei ni kuanzia miaka miaka mitano, sita mpaka saba jela, hili sio kosa la miezi miwili jela’ –Kamanda Simon Sirro

google+

linkedin