7/12/16

Rais Salva Kiir aamuru kusitishwa haraka kwa mapigano


media
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, azitaka pande zinazohasimiana kuweka silaha chini.

Nchini Sudan Kusini, Rais Salva Kiir amesaini sheria inayoamuru "usitishwaji wa uhasama haraka iwezekanavyo kuanzia saa12h00 jioni saa za Sudan Kusini (sawa na saa 9:00 saa za kimataifa), kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa katika televisheni na Waziri wa Habari, Michael Makuei.
Mapigano kati ya majeshi ya ya serikali na waasi wa zamani yalianza upya katika mji mkuu, Juba, siku tatu zilizopita.
Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa Jumatatu hii katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kati ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na vile vinavyomuunga mkono Makamu wa kwanza wa rais Riek Machar.
Ndege za kivita na vifaru vimeonekana vikitumiwa katika mapigano hayo. Hali hii imesababisha usalama kudorora katika taifa hili changa duniani, na kutishia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mapema Humatatu asubuhi Serikali ya Marekani, imetaka kusitishwa mara moja kwa vurugu nchini Sudan Kusini, baada ya kutokea mapigano mapya, jijini Juba, mapigano yanayotishia kuvunjika kwa mkataba wa amani kwenye taifa hilo jipya kabisa duniani.
Mapigano haya ni ya kwanza kati ya jeshi la Serikali na wanajeshi waasi mjini Juba, toka kurejea nyumbani kwa kiongozi wao, Riek Machar mwezi April mwaka huu, na kuchukua nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais, kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu nchini humo kwa miaka 3.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imeagiza kuondoka nchini humo kwa raia na wafanyakazi wake, na kulaani taarifa kuwa raia wa kawaida wemeshambuliwa, ambapo mpaka sasa watu 150 wamekufa kutoka kila upande. RFI
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm