7/21/16

Ripoti:Man United yamnyakua Pogpa kwa uhamisho unaovunja rekodi ya dunia


Manchester United imekamilisha dili la kumsainisha mshambuliaji wa Juventus, Paul Pogba kwa uhamisho unaovunja rekodi ya dunia, paundi milioni 100.
FBL-EURO-2016-MATCH 1-FRA-ROU
Mtandao wa Daily Mirror umeripoti kuwa United imekubali kuwalipa Juventus kiasi hicho kikubwa cha fedha ili kumchukua staa huyo wa Ufaransa kwa mkataba wa miaka mitano atakaokuwa akilipwa £210,000 kwa wiki.
Kocha wa United, Jose Mourinho, alihakikisha kuwa Pogba anajiunga na timu yake baada ya kuisaidia timu yake ya taifa Ufaransa kuingia fainali ya kombe la Euro 2016.
Chini ni uhamisho mwingine uliokuwa wa gharama zaidi katika soka.
All-Time-Most-Expensive-Player-Transfers-in-Football-History
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts