Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

7/7/16

Simu Inaweza Kuzuia Wizi wa Gari, Bodaboda


MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) ni washindi wa jumla katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

Ushindi wa Veta ni matokeo ya namna banda la mamlaka hiyo lilivyojaa vifaa vya masuala ya kiteknolojia. Veta inajivunia ugunduzi wa mambo mbalimbali yenye manufaa katika maisha ya kila siku. Wakati nchi ipo katika mchakato wa kufanya mapinduzi ya viwanda, Veta wanazidi kugundua vitu kikiwemo kifaa kitakachosaidia kuzuia wizi wa vyombo vya usafiri, zikiwemo pikipiki. Si hivyo tu, mamlaka hiyo pia imewezesha ugunduzi wa gariboti linaloweza kutembea nchi kavu na majini.

Wagunduzi katika mamlaka hiyo wanajivunia kuiwezesha nchi kuwa na vifaa vyake badala ya kuwategemea wabunifu kutoka nje. Mwalimu wa teknolojia ya mawasiliano katika chuo hicho, tawi la Kipawa jijini Dar es Salaam, Valerian Sanga anasema wamebuni kifaa cha kudhibiti wizi wa magari na pikipiki maarufu kwa jina la boda boda kwa kutumia simu. Sanga anasema, kwa kutumia kifaa hicho dereva atakuwa na uwezo wa kuzima pikipiki au gari kwa kutumia simu ya mkononi ambayo namba zake itakuwa imeingizwa katika chombo hicho.

Sanga anasema amebuni kifaa hicho kwa kushirikiana na mwalimu mwenzake wa chuo hicho anayefundisha masuala ya umeme, Christian Brighton. Kwa mujibu wa mgunduzi huyo, wametengeneza kifaa hicho kwa miaka miwili. Anasema kifaa hicho kina GPS na kinatumia mawasiliano ya simu kwa kutumia GSM itakayosaidia kujua sehemu ilipo pikipiki au gari lilipo lakini pia kinamwezesha mmiliki kuzima na kuwasha chombo hicho cha usafiri popote kilipo.

“Kifaa kama hiki kinauzwa madukani lakini kwa gharama kubwa kwa sababu unatumia simu ya mkononi ambayo namba zako zinakuwa zimefungwa katika chombo cha usafiri ili zikuwezesha kuzima kama imeibiwa, baada ya dakika tano kitazima na hakiwaki mpaka utume tena ujumbe wa kutaka iwake,” anasema Sanga. Anasema, kwa sasa wanafunga kifaa hicho kwa Sh 400, 000 lakini wanatarajia baadaye kupunguza bei baada ya kupata wateja wengi.

Sanga anasema, wanafunzi Veta wanafundishwa kutengeneza kifaa hicho ili kuongeza fursa za ajira kwa wananchi. Katika banda la mamlaka hiyo pia kuna gariboti. Mwalimu Emannuel Bukuku wa Chuo cha Veta Chang’ombe jijini Dar es Salaam ndiye aliyebuni chombo hicho. Bukuku anasema, baada ya ubunifu huo amewashirikisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika uchomeleaji na uundaji wa vyuma katika kulitengeneza.

Anasema, walianza kutengeneza gari hilo Desemba mwaka jana, na kwamba, ufungaji vifaa unaendelea na wakimaliza watafanya majaribio. “Katika umaliziaji wa vifaa vya gari hilo tutafunga vifaa vya kupiga picha na vifaa vya kisasa kwa kufanyia utafiti ndani ya maji,” anasema Bukuku. Anasema nia ya kutengeneza kifaa hicho ni kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia duniani. Bukuku anasema, gari hilo linatembea kwa kutumia mifumo inayojiendesha ya mafuta ya ‘aidiolic’na kwamba linatumia mafuta ya dizeli.

Anasema gari hilo litakuwa na mabawa kulisaidia kuelea katika maji. Kwa mujibu wa mgunduzi huyo, gari hilo linapokuwa nchi kavu linanyanyuka na likiwa baharini linashuka. “Baada ya kukamilika gari hilo litakuwa na sehemu nne ya kukaa watu na eneo maalumu kwa uchunguzi baharini hususan chini ya bahari na baadaye kutengeneza documentary,” anasema. Anawataja wanafunzi anaoshirikiana nao katika kuendelea na ubunifu huo kuwa ni Joseph Mbwilo na Mohamed Hamza.

Vijana hao ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika uchomeleaji na uundaji vyuma katika chuo cha Veta Chang’ombe. Mbali na ubunifu huo Veta, pia wametengeneza vifaa ambavyo vikiendelezwa vitasaidia kumkomboa Mtanzania bila kusubiri wabunifu kutoka nje ya nchi. Baadhi ya viongozi waliotembelea banda hilo walifurahishwa na ubunifu huo na kuahidi kusaidiana na serikali kuendeleza.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage atawezesha kupatikana kwa vibali kwa ajili ya kifaa cha kuzuia wizi wa pikipiki ili kitumike nchini. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema, kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi (COSTECH) wataendeleza ubunifu unaofanywa na mamlaka hiyo badala ya kuagiza vitu nje ya nchi. Profesa Ndalichako anasema, ni vema kifaa hicho kipelekwe Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kikaguliwe na kisha kitumike kusaidia wananchi. Anasema mbali na ubunifu, Veta pia hawakumuacha mtoto mwenye mahitaji maalumu kwa kuwa wamemwezesha kumpatia elimu ya kumwezesha kujitegemea