7/2/16

TANAPA Kuwatambua Watafiti wa Wanyama Pori

Screen Shot 2016-07-02 at 4.47.40 PM
Shirika la Hifadhi ya Taifa hapa nchini TANAPA litaendelea kuwatambua watafiti na wanasayansi ambao wamesaidia kuwafanyia utafiti wanyamapori mbalimbali katika hifadhi za taifa kwa kuwapa tuzo za heshima watafiti hao.
Meneja wa mawasilino kutoka hifadhi za taifa tanapa pascal shelutete amesema hii inaenda sambamba na maamuzi ya shirika  kumpa tuzo mwanasayansi na mtafiti dokta Jene Goodall ambae alifanya utafiti kwa zaidi ya miaka 40 tangu mwaka 1960 hadi 2000 katika hifadhi ya gombe  huku taasisi yake ikiendelea kufanya utafiti hadi sasa katika hifadhi hiyo.
Shelutete amesema tangu kuwepo kwa mtafiti huyo jene goodall ambae ni wa kwanza dunia  kufanya utafiti wa sokwe na kugundua wanashabiana  na binadamu kijenetiki kwa asilimia 98 pia mtafiti huyo  ndio alisaidia sokwe wa hifadhi hiyo kuwazoesha kushirikiana na binadamu na kuweza kutumika kwa utalii.
Naye Kaimu muhifadhi mkuu hifadhi ya gombe Dominic Talimo  amesema hifadhi ya gombe inajivunia kuwepo kwa ongezeko la watalii wa ndani ukilinganisha na watalii wa nje hii ikiwa ni njia moja wapo ya mafanikio ya watanzaia wengi kwenda katika hifadhi hiyo kuona tabia ya sokwe mtu.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm