7/26/16

TPSF kutoa mafunzo ya tovuti nchini

 
Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), wanatarajia kuendesha mafunzo maalumu kwa wajasiriamali nchini kuhusu namna ya kunufaika na tovuti mpya ya habari.
Mkurugenzi mkuu wa TPSF, Godfrey Simbeye alisema jana kuwa wameanzisha vipindi vya redio katika vituo mbalimbali mikoa ya Dodoma, Geita, Kigoma na Mbeya.
“Kampeni hii imelenga kuongeza uelewa wa wajasiriamali kuhusu tovuti hiyo yenye mifumo ya mafunzo, namna ya kuanzisha na kukuza biashara na upatikanaji wa mitaji,” alisema. Meneja mradi wa tovuti hiyo, Celestine Mkama alisema: “Tumeona umuhimu wa kuendesha kampeni ya kuongeza uelewa wa tangu wakati tunatengeneza mfumo huu wa habari.”
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts