7/19/16

Ujaji kupatikana kwa maombi
Tume ya Utumishi wa Mahakama imeamua kutangaza nafasi na ajira za majaji ili kuongeza uwazi.


Utaratibu huo wa kwanza kutumiwa na tume hiyo nchini ulianza kutekelezwa jana baada ya gazeti la serikali la Habari Leo kuchapisha tangazo hilo, likianisha sifa za kitaaluma na uzoefu zinazohitajika na uzoefu wa waombaji na viambatanisho vya uthibitisho wa sifa hizo na uzoefu wa kitaaluma vinavyohitaji.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman amesema wameamua kutumia utaratibu huo kuongeza uwazi, kupanua wigo na kuongeza ushindani ili kuwapata majaji wenye sifa.


“Huu ni utaratibu wa tume, upo kwenye tume na tumekuwa tukiuongea mara kwa mara kwenye tume, lakini tulikuwa hatujautekeleza tu. Sasa safari hii tumeona ngoja tujaribu kupanua wigo kwa kutangaza,” amesema Jaji Chande.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm