Ushuru juu kituo kikuu cha mabasi Ubungo | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

7/1/16

Ushuru juu kituo kikuu cha mabasi UbungoHALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imeongeza viwango vya ushuru kwa vyombo vya usafiri na abiria wanaotumia Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Ubungo, kuanzia Julai mosi.

Aidha, mpango wa ujenzi wa vituo viwili vya mabasi ya mkoani katika eneo la Mbezi Luis na Boko ‘umeyeyuka’ kutokana na kile kilichoelezwa halmashauri imekosa fedha kwa ajili hiyo.

Mkuu wa kitengo cha itifaki na uhusiano wa Halmashauri ya Jiji, Gaston Makwembe alitoa taarifa hiyo jana alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema wamekosa fedha za ujenzi wa vituo hivyo ambavyo, Sh bilioni 57 zilihitajika kwa kituo cha Mbezi pekee.

“Halmashauri haikuwa na fedha hizo, lakini pia bajeti inayotengewa ni ndogo masharti ya wafadhili nayo hayana unafuu, kwahiyo tumeona tuboreshe kwanza kituo cha Ubungo ila tutahakikisha tunajenga vituo bora,” alisisitiza.

Akizungumzia kupanda kwa viwango vya ushuru, Makwembe alisema awali kituo hicho kilikuwa kikisimamia uendeshaji wa shughuli zote za kituo kwa kutumia Sheria Ndogo ya Mwaka 2004 ya Kituo Kikuu cha Mabasi, hivyo kwa sasa inaanza kutumika Sheria Ndogo ya Mwaka 2009 ambayo imefuta matumizi ya Sheria ya Mwaka 2004.

Alisema Sheria hiyo ndogo ya mwaka 2009 inawataka wasindikizaji wote wa abiria watakaoingia katika kituo hicho kulipia Sh 300 badala ya Sh 200 pia magari yatakayoegeshwa vibaya yatalipishwaa faini ya Sh 15,000 badala ya Sh, 8,000 ya awali. Alisema magari yanayosafirisha abiria saba hadi 20 watalipia ushuru wa Sh 1,500 kutoka Sh 1,000 iliyokuwepo awali.

Mabasi yanayosafirisha abiria 20 hadi 28 watalipia Sh 2,500 kutoka Sh 1,500 ya awali.

Yanayosafirisha abiria zaidi ya 28 watalipia Sh 3,000 kutoka Sh 2,000 ya awali, Teksi za abiria wasiozidi wanne watalipia Sh 500 kutoka Sh 400 iliyokuwa awali.

Vyombo vingine vitakavyolipa ushuru na kiwango cha zamani kwenye mabano ni malori na matela yasiyozidi tani tatu Sh 3,000 (1,000), matela zaidi ya tani tatu Sh 5,000 (2,000), magari mengine Sh 1,000 kutoka Sh 400.

Pikipiki zitalipa Sh 300 na baiskeli Sh 200. Makwembe alisema zipo changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho, lakini halmashauri hiyo imetenga Sh milioni 463 kwa ajili ya kukarabati miundombinu .

google+

linkedin