7/22/16

Wanane wauawa katika shambulio

Polisi wakiwa eneo la tukio. Picha ya 
Ujerumani. Watu wanane wameuawa katika shambulio la risasi lililofanywa kwenye Olympia Shopping Mall jijini Munich, nchini Ujerumani.
Taarifa za awali zilizoripotiwa na maofisa wa polisi, zilisema tukio hilo lilitokea jana jioni na linahusishwa ugaidi.
Pia, taarifa hizo zilieleza kuwa watu watatu wanashukiwa kushiriki tukio hilo, ambao waliwakabili polisi kwa majibizano ya risasi na mmoja anadaiwa kuuawa.
Msemaji wa Polisi, Claudia K√ľntzel alisema watuhumiwa wafunga lango linalotizamana na uwanja wa 1972 Olympia na kwamba, kufuatia tukio hilo hatari imetangazwa hali ya hatari na wakazi wa mji huo wamewekewa amri ya kutotembea ovyo, kufungwa kwa biashara na usafiri wa umma.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm