7/19/16

Wasomi wataka mjadala wa elimu Z’bar
Wasomi visiwani Zanzibar wamesema kuna haja ya kubadili mfumo wa elimu ili kuwasaidia wanafunzi waweze kupata ufaulu mzuri.


Kwa mujibu wa matokeo ya kidato cha sita yaliyotolewa hivi karibuni, shule nyingi mashuhuri visiwani humo zimeshika mkia.


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar, Dk Mohamed Khalfan amesema kuna sababu kwa Wazanzibari kulitatua tatizo hilo kwa kuwa ni la umma, na wkamba inafaa iwe haraka iwezekanavyo.


Mtafiti wa Sayansi, Dk Rashid Slim amesema: “mwelekeo wa matokeo hayo ambayo kwa sasa siyo ya kushangaza, hauashirii matumaini yoyote ya elimu hapa visiwani.”
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts