Watoto milioni 4.2 nchini watumikishwa kiuchumi | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

7/21/16

Watoto milioni 4.2 nchini watumikishwa kiuchumi

MATOKEO ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto wa mwaka 2014 (2014 NCL), Tanzania Bara yameonesha kuwa, kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5 -17, watoto milioni 4.2 sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za kiuchumi.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk Albina Chuwa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya matokeo ya utafiti huo unaofanyika kila baada ya miaka mitano na utafiti wa mwisho ulifanyika mwaka 2006/2007.

Alisema sekta ya kilimo, misitu na uvuvi imeendelea kuongoza kwa kuajiri watoto, ikiwa na kiwango cha asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi na wengi wao wanaishi vijijini.

“Matokeo haya yameonesha kuwa watoto hutumia zaidi ya nusu ya muda wao wa siku yaani asilimia 58.8 kwa shughuli za kujihudumia na usafi binafsi, huku wasichana wakionekana kutumia muda mrefu zaidi kwa shughuli hizo, kwa kiwango cha asilimia 59.2 ikilinganishwa na wavulana wanaotumia asilimia 58.3,” alisema.

Aidha, alisema shughuli za kujisomea kwa watoto zilichukua nafasi ya pili kwa matumizi ya muda kwa kiwango cha asilimia 15.5 ambapo wavulana walitumia muda mrefu zaidi kujisomea ambao ni asilimia 16.4 ikilinganishwa na wasichana waliotumia wastani wa asilimia 14.6.

Alisema hali hiyo haiendani na kaulimbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu” kwa watoto kutumia muda mwingi katika starehe badala ya kusoma.

google+

linkedin