7/9/16

Watoto wateketea kwa moto

 
Watoto wanne wamefariki dunia baada ya nyumba waliokuwa wamelala kuteketea kwa moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema jana kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Nyerere kwenye Mji Mdogo wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa mkoani hapa wakati mtu aliyeachiwa kuwaangalia watoto kuwafungia ndani na kwenda baa.
 Amesema tukio hilo lilitokea baada ya nyumba ya vyumba sita mali ya Nelson Mdachi kuungua moto.
Amewataja watoto hao kuwa ni Elizabeth Nelson (11), Peter Lema (9), Samweli Mdachi (7) na Nase Mgomba (9).
chanzo: Mwananchi
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm