7/22/16

Watumishi vibabu ‘watafuna mbegu za vijana’

 
Wakati kukiwa na wimbi la vijana wanaomaliza vyuoni na kukosa kazi, Mkoa wa Pwani una watumishi 36 ambao  umri wao  umevuka miaka 60 waliotakiwa wawe wamestaafu lakini wanaendelea ‘kula mbegu za vijana’
Watumishi hao ni miongoni mwa 3,600 wa mkoani huo waliopo hatarini kukosa mishahara yao ya Agosti, baada ya Serikali kubaini kasoro mbalimbali katika taarifa zao.
Kati ya watumishi hao, 3,569 taarifa zao za elimu hazionekani, 36 wana zaidi ya miaka 60 lakini wapo kazini ilhali walipaswa wawe wamestaafu, sita akaunti zao hazitambuliki na 21 vyeo vyao havijabainishwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angela Kairuki alisema jana kuwa watumishi hao hawatalipwa mishahara yao hadi kasoro za taarifa zao zitakaporekebishwa.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts