7/2/16

Wezi wa Mbao za Madawati Songea mkoani Ruvuma

Wananchi wa kijiji cha Ngadinda kata ya Gumbiro wilaya Songea mkoani Ruvuma wameulalamikia uongozi wa kijiji hicho kuwa umeshiriki kula njama za wizi wa mbao za zaidi ya 1,000 zilizokuwa zitumike kutengenezea madawati ya shule za msingi na sekondari katani hapo kama ilivyoagizwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli.

Wakiongea na Channel ten kijijini hapo wananchi hao wamesema waliitika wito wa Raisi kwa kuchangia kila mwananchi shilingi elfu mbili na mia tano jambo la kushangaza viongozi wa kijjiji wamegeuza mradi huo kuwa sehemu ya kujinufaisha baada ya kupata taarifa kuwa mbao zaidi ya 1,000 ziilizochanwa zimeibiwa viongozi hao hawakuchukua hatua zozote.

Wamesema mbao zimeibiwa mara tatu kwa nyakati tofauti awamu ya kwanza 460,ya pili 370 na ya tatu 300 kati ya hizo zilizokamatwa na idara ya maliasili ni 300 na zingine zote ziliuzwa na mtu aliyetajwa kwa jina la Juma Ndango aliyekuwa mchanaji ambaye hakuwa na kibali cha kuchana mbao katika msitu wa kijiji cha Ngadinda, awamu ya kwanza kwenye gari walikuwepo wafanyakazi wa geti la ushuru wa mazao ili zivushwe bila kukaguliwa na awamu ya pili lilitumiika gari la serikali walipozuiliwa kwenye mageti walikata kamba.

Mwenyekiti wa kijiijii Sabas Mgao amekili kuwa ni kweli mbao zimeibiwa na mpasuaji licha ya mhusika kukiri wizi huo hakuna hatua za kisheria ziliizochukuliwa.

Kutokana na wizi huo mapaka sasa kata ya Gumbiro hawajachonga dawati hata moja zadi ya mgao wa madawati 40 ya halmashauri kati ya 117 yanayohitajika.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts