7/4/16

Young Dee awajibu Mtu Chee ‘sirudi kwenu asilani’Rapper Young Dee amesema suala la yeye kuwapigia magoti Stamina na Country Boy ili arudi kwenye kundi la Mtu Chee ‘halimake sense.’
13531968_1101664066571243_1094846367_n
Stamina alidai kuwa kutoka kwa Young Dee kwenye kundi hilo kulitokana na kupishana kauli kati yake na Country Boy, na kwamba kama atarekebisha makosa aliyowafanyia wako radhi kumrejesha kundini.
“Suala la mimi kwenda kuomba msamaha Mtu Chee ni suala ambalo halimake sense,” Young Dee amemuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Mtu Chee mimi pamoja na uongozi wangu sijashauriwa kabisa na sidhani kama kuna siku kutakuwa na hili kundi. Mimi niwatakie kila lakheri katika safari yao ya kimuziki na nawaombea mafanikio huko mbeleni lakini mimi suala la kurudi sidhani kama lipo tena,” amesisitiza.
Wiki iliyopita Stamina alisema: Anytime kama ataona yeye ndio alikosea kama alivyorekebisha mistakes zake katika management yake, kama ataweza kurekebisha mistakes zake pia kwenye kundi anakaribishwa anytime hakuna mtu mwenye bifu naye ni mambo tu ya kikazi na kipindi cha kati alipokuwa amechanganyikiwa na madude yake hayo kwahiyo ndio maana ilikuwa ni ngumu kuweka kukaa chini na kusolve chochote,” aliongeza.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts