66 walazwa kwa kunywa togwa harusini | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

8/28/16

66 walazwa kwa kunywa togwa harusini

Image result for togwa 
Wakazi 66 wa Kijiji cha Lyangweni wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, wamelazwa katika zahanati kwa matibabu baada ya kunywa togwa inayodhaniwa kuwa na sumu.
Afya za watu hao waliokuwa kwenye sherehe ya harusi zilibadilika ghafla juzi usiku, baada ya kuanza kuharisha na kutapika kabla ya kuwahishwa katika zahanati hiyo kutibiwa.
Hilo ni tukio la pili kutokea katika eneo hilo ndani ya miaka miwili baada ya watu wengine takriban 400 kudhurika na kinywaji hicho, Oktoba 2014.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songea, Yesaya Mwasubira amesema jana kuwa wagonjwa hao walipokewa kwa nyakati tofauti na hadi saa nane juzi usiku walikuwa wamefikia 63.
Amesema wagonjwa wengine watatu walipelekwa katika zahanati hiyo jana asubuhi baada ya afya zao kozorota.

chanzo: Mwananchi

google+

linkedin