8/28/16

Askari magereza azua kizaa zaa Hospitalini


 
 Askari wa Jeshi la Magereza mkoani hapa amezua taharuki kwa wagonjwa baada ya kuingia hospitalini na bunduki na baadaye kufyatua risasi kadhaa hewani.
Tukio hilo lilitokea wakati usalama wa askari na silaha zao, ukizidi kuwekwa kwenye hali ngumu baada ya kutokea matukio kadhaa ya polisi kuvamiwa, kuuawa na kuporwa silaha na watu wasiofahamika kudiriki kuvamia hata vituo vya polisi na kupora silaha.
Juzi usiku saa 4.00, askari jela huyo aliingia hospitali kumuangalia mwanaye aliyelazwa akihudumiwa na mkewe.
Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk John Gurisha alisema askari huyo aliingia wodi namba 10 ambako mke wake alikuwa amelazwa na mtoto.
Kamanda wa Polisi Mkoa, George Kyando amesema chanzo cha askari huyo kufanya hivyo ni ulevi uliopindukia.
Amesema mtuhumiwa anaendele kuhojiwa na atafikishwa makamani wakati wowote.
“Tunaendelea kuchunguza ili baada ya uchunguzi kukamilika, sheria ichukue mkondo wake,” amwsema Kyando. 
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm