8/29/16

Askofu Mokiwa aishauri Serikali

Askofu wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa ameishauri Serikali kuacha kuwabana watu, badala yake waruhusiwe kutoa ya ‘mioyoni’.


Askofu Mokiwa ametoa kauli hiyo jana katika mahojiano muda mfupi baada ya kuzindua kanisa jipya la Anglikana la Mtakatifu Augustino lililopo Tabata Kisukulu, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

“Hofu yangu ni kwamba watu wakiendelea kunyima haki hii wataweza kuanzisha vurugu nchini na zikitokea viongozi wa dini tutakuwa katika wakati mgumu kutoa huduma za kiroho,” amesema.


Kuhusu maandamano ya Chadema yaliyopewa jina la Ukuta, Dk Mokiwa amesema ni vyema Serikali ikazungumza na chama hicho ili kufikia mwafaka utakaokuwa na faida kwa pande zote mbili.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts