8/3/16

Basata yamnyima Snura kibaliMwanamuziki, Snura Mushi
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemnyima kibali cha kutengeneza video vya wimbo mpya mwanamuziki, Snura Mushi kwa madai kuwa hajatimiza masharti aliyopewa baada ya kufungiwa miezi mitatu iliyopita.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mwanamuziki huyo alisema ameshindwa kutengeneza video ya wimbo wake mpya Shindu baada ya Basata kumnyima kibali mpaka atakapotimiza masharti aliyopewa, moja likiwa ni kutengeneza video mpya ya wimbo Chura.
Snura alisema hivi sasa amesimamisha shughuli nyingine za muziki mpaka atakapokamilisha masharti yote kwa kuwa hawezi kupewa kibali.
Video ya wimbo Chura ilifungiwa na Serikali kwa madai ya kukiuka maadili Mei 4 mwaka huu na kuamriwa urudiwe upya ili kufuta maudhui ya awali.
Pamoja na kupewa masharti hayo, Snura hakutengeneza na badala yake alitoa wimbo mpya Shindu.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm