8/21/16

Beki Simba aanguka bafuni


BEKI mpya wa Simba, Hamad Juma amelazwa hospitali ya Mwananyamala baada ya kuanguka akiwa bafuni nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja tu tangu aisaidie timu yake kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda.
Habari zilizopatikana jioni hii zinasema kuwa  Hamad aliyetua Simba akitokea Coastal Union alianguka wakati akioga asubuhi wakati akioga na kusababisha kupasuka kisogoni ambako kutokwa damu nyingine kabla ya kukimbizwa hospitalini.
Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa madaktari wamepambana kuokoa uhai wa beki wao kwa kumuongezea damu na kumpa matibabu ya haraka na mpaka wakati anaongea na Mwanaspoti, hali ya Hamad ilikuwa inatia matumaini.
"Ni kweli mchezaji wetu alianguka bafuni na kufikia kisogoni ambako amechanika na kutokwa na damu nyingi, ila anaendelea vema japo naelekea tena hospitali kwa sasa," alisema Manara.
Mwanaspoti ilikuwa katika haraka za kwenda kumjulia hali majeruhi huyo ili kujua kinachoendelea na itawapa taarifa kamili.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm