Chadema Moshi yaunda kamati maalum | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

8/7/16

Chadema Moshi yaunda kamati maalum

Katibu wa Chadema mkoa Kilimanjaro, Basil Lema .


Chadema mkoani Kilimanjaro imeunda kikosi kazi chenye wajumbe tisa kwa ajili ya kusimamia uendeshaji wa chama hicho katika wilaya ya Moshi mjini.


Kikosi kazi hicho kimeundwa kufuatia hatua ya Baraza la Uongozi la Chadema mkoa Kilimanjaro kuivunja kamati ya utendaji ya chama hicho wilaya ya Moshi mjini wiki iliyopita kutokana na minyukano isiyoisha ndani ya kamati hiyo.


Katibu wa Chadema mkoa Kilimanjaro, Basil Lema amewataja walioteuliwa katika kikosi kazi kuwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa kamati iliyovunjwa, Jaffar Michael na Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya.


Wengine ni Abraham Kwayu, Asha Mchomvu, Adam Mtwenge, Ramso Mshiu, Abubakar Mwachitiku, Lina Mtowe na Steven Buberwa aliyekuwa Katibu wa Chadema Moshi mjini.

google+

linkedin