Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

8/10/16

Diamond atoa Millioni 20 kwa ‘GSM’ kusaidia jitihada za upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi


Msanii wa muziki Diamond Platnumz ametoa msaada wa Tsh 20 Milioni kwa ‘GSM Foundation’ kwa ajili ya kusaidia jitihada za taasisi hiyo ya kutoa huduma ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na GSM Foundation imekuwa ikizunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma hiyo bila gharama yoyote.

Raisi huyo wa label ya ‘WCB’ ameonyesha kuguswa na jitihada za taasisi hiyo na kuamua kuchangiia kiasi hicho.“Moyo wangu unaniambia nisingeshikwa mkono ama kusaidiwa na watu basi nami nisingeweza leo hii kufikia hatua hii ndogo niliofikia na ndio maana kidogo nikipatacho huwa napenda kusaidia wenzangu,” aliandika Diamond Istagram. “Leo Mapema nilitembelea ofisi za GSM foundation kuwasilisha kidogo tulichobarikiwa kwa niaba ya WCB. kwajili ya kusaidia watoto wenye matatizo ya Vichwa vikubwa (Bobble Head Syndrome) na Mgongo wazi,”

Kwa upande wa GSM Foundation, ameandika:"Leo tumepokea hundi ya shilingi milioni ishirini (20,000,000/=) kutoka kwa @diamondplatnumz kama mchango wake kwa #GSMFoundation. Tunamshukuru kwa kuja kututembelea ofisini kwetu na kwa msaada aliotupatia. Mwenyezi Mungu amuongezee pale alipopunguza."