8/23/16

Diwani: Nitaacha Kazi Wananchi Wangu wasipopata Maji.


maji
Diwani wa Kata ya Mshewe, Halmashauri ya Mbeya Vijijini,  Esther Mbega amesema ataacha udiwani kama Serikali haitapeleka maji  katika Kijiji cha Ilota ambacho  wananchi wanaamka saa 9.00 usiku kwenda kutafuta maji umbali wa kilometa 10.
Esther ameiomba  halmashauri na mkoa  kwa ujumla kuwaona kwa jicho la huruma wanakijiji hicho ili waonje matunda ya uhuru.
Akizungumza na mwandishi, diwani huyo alisema  changamoto hiyo ni kubwa na ya siku nyingi huku akisisitiza kwamba ataacha wadhifa huo kama  Serikali haitafikisha huduma ya maji safi na salama katika kijiji hicho.
“Sitaona sababu ya kuendelea na nafasi hii kama Serikali haitaona umuhimu wa kuleta maji katika kijiji hiki kwani wananchi wangu wanatabika ,ndoa zinavunjika, wajawazito wanataabika kusaka maji, “alisema.
chanzo: Mwananchi
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm