8/6/16

Dk. Cheni awachana makavu waigizaji


CHENI
MUIGIZAJI mkongwe Bongo, Mahsein Awadhi Said  ‘Dk. Cheni’ amewataka waigizaji wa Kibongo kuacha ujuaji na kukaza buti katika kufanya kazi kwa sababu wengi hawana mafanikio kivile lakini wamelewa kutokana na majina waliyonayo mitaani au kwenye media jambo ambalo yeye anafikiria kuwa haliwasaidii kabisa.
Akistorisha kupitia BBM, Dk. Cheni ambaye amesimama kuigiza kwa muda kutokana na shughuli zake za kibiashara, alisema kuwa kutokana na hali hiyo ya waigizaji kujifanya wanajua kila kitu na kuacha kujifunza jinsi gani wakomae kujikuza kisanii wamesababisha soko la filamu kuzidi kuporomoka.
“Kwa kweli waigizaji wanatakiwa kubadilika ili kufikia angalau mafanikio tuliyonayo sisi, wengi wao ni wajuaji, waache hayo mambo na wakaze buti kwenye kazi maana ndiyo msingi mzuri wa mafanikio yao,” alimaliza Dk. Cheni.

-GPL
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts