8/10/16

Dk Mwaka Ajisalimisha Polisi
Siku chache baada ya Polisi wa jiji la Dar es Salaam kutangaza kumsaka mmiliki wa iliyokuwa kliniki ya tiba asilia ya Foreplan, Juma Mwaka maarufu kama Dk Mwaka kwa agizo la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla, tabibu huyo ameamua kujisalimisha polisi.

Dk Mwaka amejisalimisha katika Kituo cha Kikuu cha Polisi, jijini Dar es Salaam na kuhojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Msako wa Dk Mwaka unachagizwa na madai ya ukiukwaji wa agizo la Serikali la kuendelea na utoaji wa tiba licha ya kufungiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdani amesema kuwa baada ya kujisalimisha muda huo, alihojiwa na kuachiwa kwa dhamana lakini akatakiwa kuripoti kwa mahojiano zaidi.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm