Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

8/22/16

Giza nene wenye vyeti feki

GIZA nene limetanda katika maisha ya siku zijazo ya watumishi wa umma walioghushi vyeti vya taaluma baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angela Kairuki, kusema ni bora wajiengue wenyewe kwenye nafasi walizonazo badala ya kusubiri kuondolewa.
Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam juzi, Waziri Kairuki alisema serikali haitamvumilia yeyote atakayebainika ameingia serikalini na cheti feki.

“Cheti feki ni jinai kwa mujibu wa kanuni za adhabu sura ya 16 ya sheria za Tanzania, hivyo watafikishwa mahakamani,” alisema.

“Hatuwezi kuvumilia cheti kimoja unakuta kimetumiwa na watumishi wawili au watatu, kwa hiyo watu hawa ni bora wajiondoe mapema," alisema Kairuki.

Waziri huyo alibainisha kuwa wapo waliofikishwa katika vyombo mbalimbali vya maamuzi, ikiwamo mahakamani kutokana na kubainika kuwa na vyeti feki "na tutaendelea kufanya hivyo."Hatuwezi kukubali watu wa namna hii kwenye serikali ya sasa.”

Kairuki alizitaka taasisi za umma kuendelea kuhimiza uhakiki wa vyeti vya watumishi katika maeneo yao.
Sakata la vyeti bandia liliibuka Bunge la 10, baada ya Mbunge wa Ole, Rajabu Mohamed Mbarouk (CUF), kuleta hoja ya kuitaka Serikali kueleza ni kwa nini Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) linashindwa kudhibiti vyeti feki.

Mbunge huyo alisema kuzagaa kwa vyeti hivyo kunaifanya hadhi ya NECTA kushuka na kukosa imani hata katika jumuiya za kimataifa.

Aidha, Mbarouk alisema vyeti feki husababisha kupata makatibu wakuu na watendaji feki. Alisema hayo baada ya wanafunzi 122 kutimuliwa katika Chuo cha Polisi Moshi kwa sababu ya kukutwa na vyeti feki.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati huo, Dk. Shukuru Kawambwa, akitoa ufafanuzi alisema NECTA baada ya kugundua udanganyifu huo ilibadilisha namna ya kuchapa vyeti ambapo sasa vina namba, jina la mhitimu katika cheti cha kuzaliwa na picha hivyo siyo rahisi kughushiwa.

Hata hivyo, Mbarouk alikataa ufafanuzi huo na kusema asilimia sita ya waomba kazi nchini wana vyeti feki na kutaka kufahamu hatua zilizochukuliwa ikiwamo za kinidhamu katika kukabiliana na suala hilo.

Kati ya watumishi 704 waliohakikiwa NECTA, watumishi 219 waligundulika kuwa waliajiriwa kwa vyeti bandia.