8/26/16

Hanscana aeleza jinsi anavyolipwa na Diamond akimshoot video zake

Mtayarishaji wa video za muziki nchini, Hanscana baada ya kufanya kazi kadhaa na Diamond Platnumz amefunguka na kuzungumzia jinsi anavyolipwa.
Hans-na-Diamond
Muongozaji huyo ambaye kwa sasa ana direct video nyingi za mastaa wa bongo, amesema anapofanya kazi na Diamond haangalii atalipwa shilingi ngapi.
“Malipo yake anayonilipa hayawezi kuwa makubwa zaidi kulinganisha na vitu ambavyo napata, nachokipata kwa Diamond ni kikubwa, ni zaidi hata akasema anilipe shilingi ngapi,” Hanscana aliambia Global TV. “Alinikutanisha na Godfather, Godfather ni director mkubwa duniani, alinikutanisha na wakurugenzi wa runinga kubwa duniani, ndio maana sasa hivi video za Hanscana zinachezwa vizuri,”
Hanscana tayari ameshafanya video kadhaa za Diamond pamoja na matangazo.
Pia muongozaji huyo amedai mpaka sasa tayari ameshafanya video za muziki zaidi ya 107 ambapo 40 kati ya hizo ni hit
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts