8/25/16

JULIO:MWADUI FC KUFUNGWA NA TOTO AFRICANS NI BARAKA


Mwanza,Tanzania.

KOCHA Mkuu wa Mwadui FC ya Shinyanga,Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema timu yake kufungwa na Toto Africans katika michezo ya ufunguzi wa msimu mpya huwa ni baraka.

Julio ametoa kauli hilo baada ya Jana Jumatano kikosi chake kuanza msimu mpya wa ligi kuu bara kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Toto Africans katika mchezo pekee wa ligi hiyo uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza.

Akifanya mahojiano na kipindi cha michezo cha TBC Taifa,Julio,amesema siku zote Mwadui FC inapofungwa na Toto Africans katika michezo ya ufunguzi huwapa mafanikio mwisho wa msimu.

Amesema "Mwaka juzi tulifungwa na Toto tukiwa daraja la kwanza katika mchezo wa ufunguzi tukapanda daraja.Mwaka jana tukafungwa tena na Toto katika ufunguzi tukafika nusu fainali ya FA Cup,leo (jana) tumefungwa tena na Toto katika ufunguzi naamini kuna mafanikio yanakuja mbele yetu".

Wakati huohuo Julio amewataka waamuzi wanaochezesha michezo ya ligi kuu bara kufuata sheria 17 za soka na siyo kuonyesha upendeleo kama ilivyokuwa katika mchezo wa jana ambapo mwamuzi alionekana kuwapendelea wenyeji Toto Africans
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts