8/8/16

Kikosi kazi kuongoza Chadema Moshi
Siku chache baada ya kuvunja Kamati ya Utendaji Wilaya ya Moshi kutokana na ‘minyukano’ isiyoisha, Chadema Mkoa wa Kilimanjaro imeunda kikosi kazi chenye wajumbe tisa kusimamia uendeshaji wa chama hicho wilayani humo.


Kikosi hicho kimeundwa baada ya Baraza la Uongozi la Chadema mkoani humo kuivunja kamati ya utendaji ya chama hicho wiki iliyopita.


Katibu wa Chadema Kilimanjaro, Basil Lema aliwataja walioteuliwa katika kikosi hicho kuwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa kamati iliyovunjwa, Jaffar Michael na Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya.


Wengine ni Abraham Kwayu, Asha Mchomvu, Adam Mtwenge, Ramso Mshiu, Abubakar Mwachitiku, Lina Mtowe na Steven Buberwa aliyekuwa Katibu wa Chadema Moshi mjini.


Lema alisema mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Phillemon Ndesamburo amewapa majukumu matatu ambayo ni kujenga misingi ya chama, kutengeneza orodha ya wanachama na kuandaa Operesheni Ukuta.


Ukuta ni operesheni yenye lengo la kupambana na kile ambacho Chadema na vyama washirika vinadai vina lengo la kupambana na udikteta Tanzania. Hata hivyo, operesheni hiyo imepigwa marufuku na polisi.

‘Minyukano’ ilivyokuwa

Katika barua ya kuvunja kamati ya utendaji ya Julai 28, mwaka huu yenye kumbukumbu CDM/KIL/IC/2016/28, Ndesamburo alisema migogoro ya muda mrefu ndani ya kamati hiyo ilikuwa inahatarisha uhai wa chama hicho.

Ndesamburo alisema baada ya kuchambua kwa umakini athari zitokanazo na mkwamo huo, baraza hilo limeamua kuivunja kamati ya utendaji ya chama hicho.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts